HII SASA IMETOKEA TANZANIA : MLEWA "HUU NDO UNYAMA ALIONIFANYIA MKE WANGU"...
![]() |
| Scina Mlewa akiwa na majeraha baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wake aitwae Habiba Shomari. |
SCINA
Mlewa (28) amejikuta akilia baada ya mke wake aliyetajwa kwa jina la
Habiba Shomari kudaiwa kumwagia uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni.
Akisimulia tukio hilo huku akilia, Mlewa alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi ni dereva wa daladala
linalofanya safari Mwenge na Temeka, Septemba 28, mwaka huu sikuweza
kurudi nyumbani baada ya basi hilo kuharibika. Kutokana na tatizo hilo,
nilishindwa kuliacha barabarani ndipo nilimtumia ujumbe mke wangu
kumuarifu.
![]() |
| Scina Mlewa akiwa na huzuni baada ya kuunguzwa kwa uji wa moto na mkewe. |
“Niliporudi
nyumbani asubuhi nilikumbana na maswali mengi kutoka kwa mke wangu,
kisha akaingia jikoni na kunyanyua surufia iliyokuwa na uji akanimwagia
usoni, ukaniunguza vibaya sana.
“Baada
kufanyiwa unyama huo nilipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo wasamaria
walikuja na kunipeleka Hospitali ya Temeke ambako nililazwa.
“Kabla
ya tukio hilo tumekuwa tukizozana mara kwa mara na hata kutishia
maisha yangu lakini nashindwa kuachana naye kwa kuwa nimezaanaye,”
alilalamika Mlewa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi wa Temeke, ACP David Misiime amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema kuwa mama huyo ameshakamatwa na upelelezi unaendelea.




No comments:
Post a Comment