Pages

Ads 468x60px

Monday, October 15, 2012

WEMA NA AUNT WAOMBA RADHI KWA WA TANZANIA

WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA KUPIGWA PICHA ZA UCHI WAKATI WA TAMASHA LA FIESTA DODOMA.



Msaanii maafuru wa filamu nchini Tanzania asiyeishiwa na vibweka Wema Sepetu (katikati) akizungumza na wanahabari katika ukimbi wa habari maelezo jijini Dar kwa nia ya kuomba radhi kwa watanzania kwa niaba yake na msanii mwenzake Ant Ezekiel kuhusiana na tukio la wao kupigwa picha zilizowaonyesha ‘ndivyo sivyo’ nusu uchi wakati wakijiachia katika Tamasha la Serengeti Fiesta lilipofanyika mkoani Dodoma. Kulia ni Msanii wa Bongo Movie Ant Ezekiel na kushoto Katibu Mkuu wa TAFF Wilson Makubi.
Msanii Maarufu wa filamu za Bongo Ant Ezekiel akisisitiza kuwa wao wameoumia sana kwa kuonekana kwa picha zile kwa sababu wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi. Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki mbalimbali wa kazi zao ambao wanawaheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria.
Wema Sepetu Mbele ya kamera ya MO Blog akiomba radhi na kusema watanzania “ Kiukweli hatujafurahia na tumeumia sana” na tunatumia fursa hii kuomba Msamaha.
Moja ya picha ya Msanii Aunty Ezekiel iliyosamba kwenye mitandao ya Kijamii hivi karibuni wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Saturday, October 13, 2012

PICHA ZA VURUGU ZA MBAGALA

Hapa baadhi ya waislamu walioamua liwalo naliwe na kuamua kuwatunishia msuli polisi na kusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.
Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vuru.
Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani.
Waisilamu waliotoka msikitini kwenye swala ya Ijumaa walikumbana na kimbembe cha kamatakamata hatakama hawakuwemo kwenye sakata hilo, alama ni kanzu na sijda


Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira.
Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo.
Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka.
Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.

 Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate.


 Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo


 Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)



 Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam leo



HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR 



VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.



Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.



Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.



Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.



Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.



Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.



Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.



“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa 

KIJANA AJINYONGA MAENEO YA SINZA KWA REMMY

BREAKING NEWS: KIJANA AJINYONGA MAENEO YA SINZA KWA REMMY, (tunaomba radhi kwa picha utakazoziona)

 Mwili wa marehemu Kassim Athuman ukiwa umening’inia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani chumbani kwake leo, tukio hili limetokea kwenye mtaa wa Sinza ‘E’, kata ya Sinza Wilaya ya Kinondoni amekutwa amejinyonga chumbani kwake mapema jioni ya leo.
 Shaban Athuman ambaye ni kaka wa marehemu akitoa maelezo kwa afisa polisi aliyefika kuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi
 Picha ya marehemu Kassim enzi za uhai wake
ni kilio na majonzi kwa ndugu jamaa na marafiki

Wednesday, October 10, 2012

MWANAMKE AMWAGIA MUMEWE UJI WA MOTO USONI

HII SASA IMETOKEA TANZANIA : MLEWA "HUU NDO UNYAMA ALIONIFANYIA MKE WANGU"...



Scina Mlewa akiwa na majeraha baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wake aitwae Habiba Shomari.

 SCINA Mlewa (28) amejikuta akilia baada ya mke wake aliyetajwa kwa jina la Habiba Shomari kudaiwa kumwagia uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni.


 Akisimulia tukio hilo huku akilia, Mlewa alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi ni dereva wa daladala linalofanya safari Mwenge na Temeka, Septemba 28, mwaka huu sikuweza kurudi nyumbani baada ya basi hilo kuharibika. Kutokana na tatizo hilo, nilishindwa kuliacha barabarani ndipo nilimtumia ujumbe mke wangu kumuarifu.


Scina Mlewa akiwa na huzuni baada ya kuunguzwa kwa uji wa moto na mkewe.
“Niliporudi  nyumbani asubuhi nilikumbana na maswali mengi kutoka kwa mke wangu, kisha akaingia jikoni na kunyanyua surufia iliyokuwa na uji akanimwagia usoni, ukaniunguza vibaya sana.



“Baada kufanyiwa unyama huo nilipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo wasamaria walikuja na kunipeleka Hospitali ya Temeke ambako nililazwa.

“Kabla ya tukio hilo tumekuwa tukizozana mara kwa mara na hata kutishia maisha yangu lakini nashindwa kuachana naye kwa kuwa nimezaanaye,” alilalamika Mlewa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,  ACP David Misiime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mama huyo ameshakamatwa na upelelezi unaendelea.

MWILI WA ALIYE KUWA KIONGOZI WA WAUZA UNGA WAIBWA MEXICO

HII KALI: MWILI WA MKUU WA KUNDI LA WAUZA ‘UNGA’ MEXICO ALIYEUAWA WAIBIWA.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida maiti ya mmoja wa viongozi wa mtandao wa madawa ya kulevya waliokuwa wakitafutwa sana nchini Mexico Heriberto Lazcano aliyeuawa umeibiwa kutoka katika nyumba yalikokuwa yakifanyikia mazishi yake.
Rais wa Mexico Felipe Calderon amelipongeza jeshi kwa operesheni iliyofanikisha kuuawa kwa Lazcano, aliyekuwa mkuu wa kundi la Zetas ambalo limefanya mauaji ya kikatili, katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini Mexico.
Takriban watu elfu 60 wameshauawa katika mgogoro kati ya makundi mbali mbali ya madawa ya kulevya na polisi tangu Rais Calderon aingie madarakani mwaka 2006.

MADHARA ANAYOWEZA KUPATA MTU ANYEPENDA KUCHATI MARA KWA MARA

Angalizo muhimu sana: Haya ndiyo madhara unaweza kuyapata wewe unayependa kuchat kwa simu kila muda.. soma hapa uelimike



PHILADELPHIA (CBS) – If you’re an active cell phone user, you may be developing a growing health condition: texting thumb.
According to Jefferson University Hospital, texting thumb—a form of tendinitis in the thumbs—is one of the most common ailments seen by hand specialists today.
Dr. Eon Shin, a Jefferson orthopedic surgeon, says the increasing use of cell phones and computers have led to the overuse of our hands and wrists, leading to a rise in “techno-injuries,” especially among gen-Xers.
Fortunately, texting thumb can be treated fairly simply.
According to Dr. Shin, most people with texting thumb can treat it with simple rest or physical therapy.
Those with more serious conditions can undergo a procedure that requires a ½-inch incision in the bottom of the thumb that allows the inflamed tendon to move more freely.
It may be easy to overlook the symptoms, but those experiencing tingling or numbness in the hands are urged not to ignore it or think of it as a normal bodily occurrence.
As easy as it may be to treat texting thumb, according to Dr. Shin, the best way to avoid it is to lay off the phone from time to time.
cbslocal

You might also like:

BLOG MBALI MBALI